Katibu
tawala wa mkoa wa Shinyanga Bw.Abdul Dachi amemuagiza mkurugenzi wa
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga Eng.Sylvester
Mahole kuhakikisha mfumo wa uondoaji wa maji taka katika mji huo
unajengwa na kuanza kutumika haraka iwezekanavyo kwakuwa ukosefu wa
miundombinu hiyo unachangia kutokea mlipuko wa magonjwa ya matumbo mara
kwa mara ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga
Bw.Abduli Dachi katika ziara ya kushtukiza aliyofanya katika ofisi za
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga ambapo alibaini
changamoto kadhaa zinazokwamisha mamlaka hiyo kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Katika hatua nyingine katibu Dachi ametembelea ofisi za bonde la
maji kanda ya kati na kushtushwa na mrundikano wa vyuma chakavu na
majengo yaliyochakaa katika eneo hilo ambapo alilazimika kutoa amri ya
kuondolewa vyuma hivyo ili kupisha nafasi kwa ofisi za mamlaka ya maji
safi na usafi wa mazingira Shinyanga kuhamishia ofisi zake katika maeneo
hayo.
Awali kabla ya maagizo ya katibu tawala mkurugenzi wa mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira mkoani Shinyanga Eng.Sylvester Mahole
ameeleza baadhi ya changamoto zinazokwamisha mamlaka hiyo ikiwa ni
pamoja na baadhi ya taasisi za serikali kutolipia ankara za maji na
uhaba wa watumishi na vitendeakazi.
No comments:
Post a Comment