Jamii
imetakiwa kuwa na moyo wa kuwasaidia watoto wamitaani kwa kuwapatia
mahitaji muhimu ikiwa pamoja na kuwashawishi kuwenda shule, kwa kufanya
hivyo taifa baadaye litakuwa limepunguza idadi kubwa ya vijana ambao
watakuwa hawana shuguli maalumu za kufanya ikiwemo wanojihusisha na
vitendo vya uhalifu.
Hayo amesema mkuu wa kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha
Chrildren Community Center cha mjini Singida Sister Sara Emmanuel baada
ya viongozi wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Singida
kutoa msaada kwa watoto hao zaidi ya miatano ambao wanalelewa na kituo
hicho.
Akitoa msaada huo mwenyekiti wa shirikisho hilo Bi Mary Mpoke
amesema wanafunzi wameguswa na kuwaonea huruma watoto hao ambao ni
viongozi wa baadaye na kuamua kuwa changia kutoka katika posho zao za
kujikimu chuoni na kwa kuwanunulia mikate, vifaa vya usafi, sabauni,
madaftari.
Kituo hicho ambacho kipo Singida mjini kimekuwa kikitoa msaada kwa
kuwapatia chakula na mahitaji mengine ya shule kila siku wanapotoka
shuleni kwa mashariti ya kuonyesha walicho soma kwa siku, kikiwa na
lengo la kuwa shawishi kuendelea na masomo kwa kwenda shule badala ya
kuzurura na kuwa watoto wa chokoraa.
No comments:
Post a Comment