Mgomo huo umeanza majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo kwa
wafanyakazi hao kukusanyika nje ya lango kuu la kuingia ndani ya kambi
hiyo ya wakandarasi kutoka China iliyopo katika kijiji cha Nyakabindi
wilayani Bariadi.
Baadhi ya wafanyakazi hao wakizungumza kwa hisia, baada ya askari
wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu kuwasili katika eneo
hilo kwa lengo la kuwatawanya walikuwa na haya ya kusema.
Afisa raslimali watu wa kampuni hiyo Rosemary Mayunga, alipotakiwa
na ITV kuzungumzia madai ya wafanyakazi hao aliamua kugeuka bubu huku
akificha sura yake mbele ya kamera ya ITV.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amelitolea
ufafanuzi suala hilo baada ya kukutana na uongozi wa kampuni hiyo,
wawakilishi wa wafanyakazi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo
ofisini kwake.
Ujenzi wa barabara ya Lamadi hadi Bariadi uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 67, ulianza Oktoba mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment