Friday, May 20, 2016

CWT kuwaendeleza walimu wake katika taaluma ili kukidhi viwango vya kuwa viongozi wa Serikali.



Chama wa Walimu Tanzania (CWT) kimesema kitaendelea kufanya jitihada za kuwaendeleza walimu wanawake   katika taalum  ili wakidhi viwango na sifa za kuwa viongozi wa serikali, taasisi na mashirika ya umma katika zama za sasa ambazo serikali inaendelea kutekeleza mipango ya mgawanyo sawa wa madaraka na uo ngozi yaani Hamsini kwa Hamsini.
Aki zungumza  na kitengo cha walimu wanawake wa CWT kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaokutana Mjini Dodoma kujadili  matatizo yanayo wakabili walimu,Makamu Mwenyekiti wa CWT,LEAH UTAYA amewataka walimu wanawake wasibaki nyuma katika kujiendeleza  katika taalum ili wa shiriki katika shughuli za kitaaluma na shughuli za ujenzi wa taifa kwa kuzingatia kwamba kada ya walimu na hasa wanawake ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watumishi wengi wa serikali .
 
Nao baadhi ya walimu akiwemo Mwenyekiti wa kitengo cha walimu wanawake CWT taifa ,   SHANDA MTAKI amesema pamoja na kwamba walimu wanawake wanakabiliwa na  matatizo mengi,  lakini bado kuna fursa nyingi za maendeleo kwao .
 

No comments:

Post a Comment