Jose Mourinho anayetarajiwa kuwa kocha mpya wa Manchester United (kushoto pichani) anatarajiwa kumpatia kazi nyingine kwenye benchi la ufundi Ryan Giggs (kulia pichani).
Jose Mourinho anajiandaa kumtafutia kazi nyingine ya kufanya Ryan Giggs, kwenye benchi lake la ufundi, lakini si kuwa kocha msaidizi wa Mreno huyo.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari nchini Uingereza, Mourinho anataka kufanya kazi na msaidizi wake anayemuamini Rui Faria.
Mazungumzo ya Mourinho na Manchester United kabla ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo, yanatarajiwa kufanyika hii leo, ambapo wakala wa kocha huyo Jorge Mendes atakutana na Makamu Mtendaji Mkuu wa Mashetani hao wekundu, Ed Woodward Jijini London.