Friday, May 20, 2016

Yanga: TFF wametupa Kombe feki.



yanga ubingwaNa Wilbert Molandi
YANGA wamelipokea Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini uongozi wa timu hiyo umeibuka na kudai Kombe hilo halina hadhi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerrry Muro alisema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadhamini wa ligi kuu hiyo wanatakiwa kuboresha makombe yao watakayoyatoa kwenye misimu ujao.
chaMuro alisema ni vema likawa na muundo mmoja wa kombe litakalofanana na atakalopewa bingwa na siyo kila msimu kubadilishwa muundo wa makombe na kwamba la msimu huu haliendani na la msimu uliopita ambalo ni dogo.
“Nimeliangalia hili kombe letu tulilopewa na TFF, kiukweli halina hadhi ya kupewa bingwa, kwani hadi hivi sasa limechubuka mara tatu katika sehemu mbalimbali.
“Hivyo, nawashauri TFF na wadhamini wetu wa ligi ni vema wakariboresha kombe hilo, pia ni lazima liwepo moja litakalofanana na siyo kubadilishwa kila msimu.
“Ukiangalia kombe hili tulilopewa kwenye msimu huu ni tofauti na la msimu uliopita ambalo ni dogo, hivyo lazima liwepo kombe la ligi la muundo mmoja litakalofanana kama ‘gold’, ‘diamond’ au dhahabu, lakini siyo kama hili,” alisema Muro.

No comments:

Post a Comment