Chama
wa Walimu Tanzania (CWT) kimesema kitaendelea kufanya jitihada za
kuwaendeleza walimu wanawake katika taalum ili wakidhi viwango na
sifa za kuwa viongozi wa serikali, taasisi na mashirika ya umma katika
zama za sasa ambazo serikali inaendelea kutekeleza mipango ya mgawanyo
sawa wa madaraka na uo ngozi yaani Hamsini kwa Hamsini.
Aki zungumza na kitengo cha walimu wanawake wa CWT kutoka mikoa
mbalimbali nchini wanaokutana Mjini Dodoma kujadili matatizo yanayo
wakabili walimu,Makamu Mwenyekiti wa CWT,LEAH UTAYA amewataka walimu
wanawake wasibaki nyuma katika kujiendeleza katika taalum ili wa
shiriki katika shughuli za kitaaluma na shughuli za ujenzi wa taifa kwa
kuzingatia kwamba kada ya walimu na hasa wanawake ndiyo inayoongoza kwa
kuwa na watumishi wengi wa serikali .
Nao baadhi ya walimu akiwemo Mwenyekiti wa kitengo cha walimu
wanawake CWT taifa , SHANDA MTAKI amesema pamoja na kwamba walimu
wanawake wanakabiliwa na matatizo mengi, lakini bado kuna fursa nyingi
za maendeleo kwao .
No comments:
Post a Comment