YANGA wamelipokea Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini uongozi wa timu hiyo umeibuka na kudai Kombe hilo halina hadhi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerrry Muro alisema
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadhamini wa ligi kuu hiyo
wanatakiwa kuboresha makombe yao watakayoyatoa kwenye misimu ujao.
Muro
alisema ni vema likawa na muundo mmoja wa kombe litakalofanana na
atakalopewa bingwa na siyo kila msimu kubadilishwa muundo wa makombe na
kwamba la msimu huu haliendani na la msimu uliopita ambalo ni dogo.
“Nimeliangalia hili kombe letu
tulilopewa na TFF, kiukweli halina hadhi ya kupewa bingwa, kwani hadi
hivi sasa limechubuka mara tatu katika sehemu mbalimbali.
“Hivyo, nawashauri TFF na wadhamini wetu
wa ligi ni vema wakariboresha kombe hilo, pia ni lazima liwepo moja
litakalofanana na siyo kubadilishwa kila msimu.
“Ukiangalia kombe hili tulilopewa kwenye
msimu huu ni tofauti na la msimu uliopita ambalo ni dogo, hivyo lazima
liwepo kombe la ligi la muundo mmoja litakalofanana kama ‘gold’,
‘diamond’ au dhahabu, lakini siyo kama hili,” alisema Muro.
No comments:
Post a Comment