Hamad ameyasema hayo siku chache mara baada ya kuanza kazi ofisini kwake ambapo pamoja na mambo mengine ameshiriki zoezi la kupanda miti kwa lengo la kutunza mazingira.
''Wanaoamini watashiba kwa kufanya siasa ofisini watuachie ofisi waende kwenye siasa kwenye maeneo wanayotaka lakini sasa kwenye eneo langu ni kazi tuu na mnanifahamu mimi ninapenda uwajibikaji na si siasa kazini''
- Amesisitiza Hamad.
Aidha amewasisitiza wananchi kwamba wakati wa kufanya siasa umekwisha visiwani humo na kilichobakia ni kuwatumikia wananchi, kiongozi huyo wa chama cha upinzani alichaguliwa na Rais Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa waziri wa kilimo ambapo katika uchaguzi wa marudio uliopita alishika nafasi ya tatu kwa kupata wa asilimia tatu ya kura zilizopigwa kisiwani humo.