Wednesday, April 13, 2016

Wakiwafyatulia risasi jibuni mapigo-Acp Msangi.


Kamanda mpya wa Mkoa wa Mwanza ACP, Ahmed Msangi, amewataka askari wake kutumia mbinu za kijeshi kudhibiti vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha za moto ili kukomesha kabisa matukio ya aina hiyo katika mkoa huo.
Kamanda mpya wa Mkoa wa Mwanza ACP, Ahmed Msangi,
Akizungumza wakati akikaribishwa katika mkoa huo Kamanda Msangi, amewataka askari hao kujibishana kwa silaha endapo watakua wanakabiliana na majambazi wenye silaha ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwa askari na jamii kwa ujumla.
Kamanda Msangi amesema kuwa haikubaliki askari kupambana na Majambazi wanaotumia silaha kwa kupambana na marungu na kusisitiza kuwa yoyote atakaetumia uhalifu wa silaha achapwe kwa silaha vilevile.
Aidha, Kamanda huyo wa Mwanza amewataka askari hao kuumpa ushirikiano wa karibu kwa kufanya kazi ikiwa ni kuendana sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano na ikiwezekana wazidishe kasi zaidi.

No comments:

Post a Comment