Monday, April 11, 2016

Zaidi ya wafanyakazi 300 wa kampuni ya ujenzi wa barabara Bariadi wamegoma.

Zaidi ya wafanyakazi 300 wa kampuni ya China Communications Contrustions Ltd (CCCC), inayojenga barabara yenye urefu wa kilometa 71.8, kuanzia Lamadi hadi Bariadi kwa kiwango cha lami, wamegoma kuingia kazini wakimtaka mwajiri wao kuwalipa mapunjo pamoja na malimbikizo yao ya mishahara ya miaka mitatu na kupinga kitendo cha baadhi yao kufukuzwa kazi kiholela bila kulipwa stahiki zao.
Mgomo huo umeanza majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo kwa wafanyakazi hao kukusanyika nje ya lango kuu la kuingia ndani ya kambi hiyo ya wakandarasi kutoka China iliyopo katika kijiji cha Nyakabindi wilayani Bariadi.
 
Baadhi ya wafanyakazi hao wakizungumza kwa hisia, baada ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu kuwasili katika eneo hilo kwa lengo la kuwatawanya walikuwa na haya ya kusema.
 
Afisa raslimali watu wa kampuni hiyo Rosemary Mayunga, alipotakiwa na ITV kuzungumzia madai ya wafanyakazi hao aliamua kugeuka bubu huku akificha sura yake mbele ya kamera ya ITV.
 
Hata hivyo, mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amelitolea ufafanuzi suala hilo baada ya kukutana na uongozi wa kampuni hiyo, wawakilishi wa wafanyakazi na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ofisini kwake.
 
Ujenzi wa barabara ya Lamadi hadi Bariadi uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 67, ulianza Oktoba mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment