Saturday, June 11, 2016

Bajeti mbadala ya upinzani ni Tsh trilion 22.49



Kambi rasmi ya upinzani Bungeni leo imewasilisha hotuba yake kuhusu hali ya uchumi wa taifa , mpango wa maendeleo wa taifa na makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, huku ikiwa na wasiwasi katika baadhi ya manunuzi ikiwemo ununuzi wa ndege zinazotarajiwa kununuliwa kuwa sio mpya.
Hotuba hiyo imewasilishwa na msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na naibu waziri kivuli wa fedha na mipango Mh. David Silinde amesema kuwa Serikali imedanganya bunge kwa kuleta bajeti zinazokinzana katika vitabu vya bajeti na bajeti kuu.
Wakati huo huo kamati ya bunge ya bajeti kupitia kwa mwenyekiti wake Hawa Ghasia pia imesoma taarifa yake kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2015 na mpango wa taifa wa maendeleo kwa mwaka 2016/2017 , tathmini na utekelezaji wa bajeti ya serikali, mapato na matumizi kwa mwaka 2016/2017 inayoonesha kupongeza bajeti iliyopangwana serikali.
Katika taafa hiyo, kamati imeelezea kusikitishwa na kitendo cha serikali kupuuza maoni ya kamati hiyo jambo lililoifanya bajeti hiyo iwasilishwa bila kuzingatia maoni ya kamati.
Hii ndiyo sura halisi ya bajeti mbadala kutoka kwa kambi rasmi ya upinzani bungeni
A: Mapato ya ndani ya Kodi na yasiyo ya kodi 18,172,736,200,000/-
B: Mapatoya Halmashauri 817,773,129,000/-
JUMLA MAPATO YA NDANI 18,990,509,329,000/-
C: Mikopo na misaada ya mashart nafuu 383,002,000,000
D: Misaada na Mikopo ya miradi 2,745,659,000,000
E: Misaada na mikopo ya Kisekta 372,147,000,000
JUMLA YA MIKOPO NA MISAADA YA NJE 3,500,808,000,000/-
JUMLA YA MAPATO YOTE 22,491,317,329,000/-
MATUMIZI
E: Matumizi ya Kawaida 15,410,000,000,000/-
(i).Deni miradi ya maendeleo 8,000,000,000,000/-
(ii).Mishahara 6,600,000,000,000/-
(iii) Matumizi mengineyo
a. Wizara 360,000,000,000/-
b. Halmashauri 450,000,000,000/-
H: Matumizi ya Maendeleo 7,081,317,329,000/-
1. Kukuza Uchumi Vijijini (35%) 2,478,461,065,150/-
2. Huduma za Jamii (28%) 1,982,768,852,120/-
3. Miundombinu (17%) 1,203,823,945,930/-
4. Usimamizi wa Ardhi (12%) 849,758,079,480/-
5. Utalii (8%) 566,505,386,320/-
JUMLA YA MATUMIZI YOTE 22,491,317,329,000/-

No comments:

Post a Comment