Thursday, June 9, 2016

Malawi yaridhishwa na huduma za afya zitolewazo Tanzania.



Nchi ya Malawi imesema kuwa imeridhishwa na huduma za afya zinazotolewa nchini Tanzania kwani kumekuwa na mpangilio mzuri wa mawasiliano baina ya idara moja na nyingine sambamba na uongozi imara.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa wizara ya Afya nchini Malawi Bi Chimwemwe Gloria Banda alipotembelea nchini Tanzania akiwa ameongozana na wakurugenzi wa idara za afya tatu kwa lengo la kujifunza muundo wa utekelezaji wa shughuli za uhakiki ubora wa huduma katika sekta ya afya nchini Tanzania.
Bi Banda amebainisha kuwa nchini Malawi wameanzisha kitengo cha uhakiki ubora hivyo wameona waje nchini kuangalia jinsi ambavyo Tanzania imefanikiwa katika mpango huo ili na wao waweze kufanikiwa.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara ya Afya Dkt Mohamed Ally Mohamed amesema kuwa hivi sasa nchi ya Tanzania na Malawi zimeweka sawa miongozo itakayowawezesha kurahisisha huduma za matibabu baina ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment