Friday, June 10, 2016

Diamond aunga mkono kutozwa milioni 10 plate namba.


Kufuatia hotuba ya serikali kuonyesha hivyo kipindi cha EADRIVE kinachorushwa na EA Radio kimeongea na msanii Diamond Platnumz kuhusu mkakati huo ikiwa yeye ni mmoja wa wanaolengwa na jambo hilo.
Akijibu swali hilo msanii huyo amesema mtu anayetaka kuweka Plate Number ya jina lake maana yake anafedha zilizokithiri na kama anafedha zilizokithiri bora serikali ichukue fedha hizo ikasaidie watu wengine.
‘’Kama serikali itatumia fedha hizo kusaidia watu wa hali ya chini mimi naona sawa tuu’’ amesema Diamond.

No comments:

Post a Comment