Sunday, January 24, 2016

Asilimia 50 ya watoto mkoani Mbeya wabainika kuwa na udumavu wa mwili na akili.

Licha ya kuwa na vyakula vingi na matunda ya kutosha, mkoa wa Mbeya una asilimia 50 ya watoto wenye udumavu wa mwili na akili, hali ambayo inadaiwa kusababishwa na mila potofu zinazohusisha malezi ya mimba na watoto wenye umri wa chini ya miezi sita.
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya afya mkoani Mbeya, mratibu wa uzazi na watoto mkoa wa Mbeya, Prisca Butuyuyu amesema kuwa utafiti ambao umefanyika unaonyesha kuwa mkoa wa Mbeya unaongoza nchini kwa kuwa na asilimia 50 ya watoto wenye udumavu wa mwili na akili ukiwa juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 42.
 
Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina amesema kuwa tayari mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayosaidia watu masikini na wenye uhitaji mkubwa, CRS, umeshaandaa mkakati wa miaka mitano wa kukabiliana na tatizo la udumavu wa mwili na akili kwa watoto watakaozaliwa, mpango ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hilo akifungua mkutano huo, katibu tawala mkoa wa Mbeya, Mariam Mutunguja amesema mkoa wa Mbeya unavyo vyakula vingi ambavyo vikitumika vizuri hakuna sababu ya kuwepo kwa tatizo la udumavu, lakini akadai kuwa chanzo cha tatizo ni mila potofu zinazofuatwa na akinamama wanapopata ujauzito, hivyo akawataka wataalam wa afya kuwatumia watu maarufu na machifu kufikisha elimu ya kupambana na mila hizo.

No comments:

Post a Comment