Sunday, January 24, 2016

Watu 2 wamefariki dunia na kaya zaidi ya 20 hazina makazi kutoka na mvua zinazonyesha Kigoma.

Watu wawili wamekufa huku zaidi ya kaya ishirini zikikosa makazi katika wilaya ya Kigoma kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambazo pia zinahatarisha majengo kadhaa kubomoka.
Watu hao wanaripotiwa kufa katika kijiji cha Zashe kata ya Kagunga katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma huku mva hiyo ikikata mawasiliano katika vitongoji vya Rusollo, Bukombe na Mlama, ambapo akiongea kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amekiri mvua kusababisha vifo na uharibifu huo.
 
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Kigoma ujiji ambako pia mvua imesababsha madhara makubwa na kuacha familia kadhaa bila ya makazi pamoja na kuhatarisha majengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jingo la shirika la nyumba la taifa NHC wamewalalamikia wakandarasi na kuomba serikali kujenga miundombinu imara ili kuelekeza maji katika ziwa Tanganyika.
  
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kigoma mjini Hussein Kalyango amesema ujenzi wa daraja la Stesheni na miradi mingine ya kuwezesha mji huo kupitisha maji imechelewa na kusababisha adha kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment