Tuesday, January 26, 2016

Zile Picha za Mwanamke Aliyekutwa Shimoni Hakuwa Msukule, Ndugu Wamesimulia.

Kulikuwa na picha mitandaoni zilizoenea, wako waliosema mwanamke huyo aliyekutwa maeneo ya Kibamba Dar ni msukule… wengine wakasema ana matatizo ya akili.

Hekaheka ya jana radio Clouds FM ilisikika na stori kuhusu jinsi mwanamke huyo alivyokutwa ndani ya shimo na mwenye nyumba, Polisi wakamchukua baadae akawapotea katika mazingira ya kutatanisha.

Stori kwenye Hekaheka leo wamepatikana ndugu, pamoja na mume wa mwanamke huyo… wamesema imepita kama wiki nne toka amepotea, ni kweli ana matatizo ya akili lakini hakuwahi kuwa kwenye hali mbaya kiasi cha kutojitambua.

Ndugu hao wamesema mwanamke huyo ana watoto wawili, alipotea baada ya kwenda kwa mama yake maeneo ya Tabata, na mama yake hakutoa ushirikiano mzuri baada ya mwanamke huyo kupotea huku akisingizia anaumwa.

No comments:

Post a Comment