KWA MARA NYINGINE tunakutana hapa kuweza kupeana darasa huru la mahaba. Hapa huwa tunajadili pamoja mada mbalimbali ambazo kimsingi zinaweza kuwa changamoto kwa wengine lakini kupitia wao tunajifunza pamoja.
Bila kupoteza muda, wiki hii tunajadili
mada iliyopo mezani. Usaliti unauma. Hakuna ambaye atafurahia pindi
asikiapo mwenzake amemsaliti. Ndiyo maana wapendanao hutumia nguvu
nyingi sana kuhakikisha tu mwenzake hamsaliti.
Wapo ambao wanadiriki hata kuwawekea
ulinzi wenza wao ili kuhakikisha kwamba kila kitakachofanywa na mpenzi
wake anakijua. Kila eneo atakapokuwa mpenzi wake kunakuwa na watu
wanaofikisha habari kama zilivyo.
Kundi la wanaume au wanawake wa aina
hiyo ndiyo wale wanaokosa ustamilivu. Akimuona mpenzi wake amesimama na
mtu tu barabarani, hana imani. Anatamani kujua wanazungumza nini. Mpenzi
wake akichelewa kurudi nyumbani, anatilia shaka.
Anapiga simu kila dakika. Anamuuliza yuko wapi. Ikiwezekana amfuate hapo alipo ili kama kuna figisufigisu zozote amfumanie.
Anapiga simu kila dakika. Anamuuliza yuko wapi. Ikiwezekana amfuate hapo alipo ili kama kuna figisufigisu zozote amfumanie.
Akiwa amekaa pamoja na mpenzi wake
anakosa amani. Simu ya mpenzi wake ikiita, anatega sikio haraka
kusikiliza anayezungumza naye ni nani.
Kukagua simu kila wakati. Anataka kuona
kama kuna madudu. Kila wakati anawapigia marafiki wa mpenzi wake, kujua
taarifa za mtu wake. Hiyo ndiyo staili ya maisha yake. Matokeo yake
inageuka kero kubwa kwa yule anayefuatiliwa.
Hapo ndipo zinapoibuka kauli kama hizi;
“Huyu naye amezidi bwana. Haiwezekani awe ananichunga kama mbuzi. Mimi
ni mtu mzima. Najua mema na mabaya. Bora hata ingekuwa kweli nafanya
madudu lakini sifanyi. Yeye kila siku ananifuatilia.
“Nakosa
uhuru. Kila unachofanya unajua nafuatiliwa. Kila ukifanya kitu
anakitilia shaka. Bora hata tuachane maana kwa staili hii tutakuwa watu
wa kugombana kila kukicha.”
Marafiki zangu, hapa kuna kitu cha
kujifunza. Kuna umuhimu mkubwa wa kuishi na mtu unayemuamini. Mwanadamu
huwezi kumchunga. Kama mtu una shaka naye ni bora kuachana naye.
Kila mmoja wenu anapaswa kujitambua.
Akili ya kujitambua kila mwanadamu amepewa na Mungu. Kutambua wewe ni
nani na huyo mliyenaye mna malengo naye gani? Jadilini pamoja kuhusu
umuhimu wa kujitambua.
Kama mna malengo ya kuishi kama mke na
mume, heshima ya mume na mke ni nini? Mume ajitambue kwamba anapaswa
kulinda utu wa mwenzi wake, vivyo hivyo kwa mke.
Hakuna kinachobadilika kwenye mapenzi. Kila unachokihitaji kwa maana ya mahitaji ya mwili, mpenzi wako anacho.
Hakuna kinachobadilika kwenye mapenzi. Kila unachokihitaji kwa maana ya mahitaji ya mwili, mpenzi wako anacho.
Hakuna sababu ya kuwa na tamaa. Ridhika
na kile unachokipata kutoka kwa mpenzi wako. Uone kwamba unaposaliti ni
kama mpenzi wako anakuona unachokifanya. Utambue kwamba kuna maradhi
pia. Kuchepuka ni aibu. Ni kumdhalilisha yule umpendaye. Kama unampenda
kweli kwa nini umsaliti? Mnapaswa kukubaliana kwamba hakuna sababu ya
kuchungana lakini kila mmoja wenu ajichunge e ni mwenyewe .
N jia ya muongo siku zotfupi. Huna sababu ya kumchunga sana mpenzi wako kwani ipo siku ataumbuka yeye mwenyewe. Ikitokea hivyo mtazungumza na akiomba msamaha na kuahidi kutorudia, msamehe na umpe nafasi nyingine.
N jia ya muongo siku zotfupi. Huna sababu ya kumchunga sana mpenzi wako kwani ipo siku ataumbuka yeye mwenyewe. Ikitokea hivyo mtazungumza na akiomba msamaha na kuahidi kutorudia, msamehe na umpe nafasi nyingine.
Nisisitize kwamba hakuna sababu ya kuchungana, kila mmoja ajichunge mwenyewe kwa kujiwekea uaminifu kwa mwenzake!
No comments:
Post a Comment