1. Jipu Latumbuliwa NIDA..
Hii ni habari inayopewa nafasi ya kwanza kwa uzito na mtandao waMjengwablog.com.
Mimi kama
mwandishi wa makala nilipata kuliandikia hili la NIDA kwenye safu yangu
ya gazetini Raia Mwema mwezi Agosti, 2011. Niliandika haya kwa kichwa
cha makala kinachosemeka hapo chini;
' Mradi wa vitambulisho ni kioja kingine!'
"NI
Mwanafalsafa yule wa Kiyunani, Ptolemy aliyepata kuandika; ”Ex Africa
simper aliquid novi". Maana yake: "Kila kukicha kitazuka kioja kingine
Afrika."
Katikati
ya dhahma hii ya kiuchumi tuna mfano wa vipaumbele vya Serikali
vinavyotia hasira. Mojawapo ni huu unaoitwa Mradi wa Vitambulisho vya
Kitaifa. Mchakato wake umeanza tangu mwaka 2007. Ni baada ya Baraza la
Mawaziri kuubariki Februari 2 mwaka huo. Mwakani mchakato huu utatimiza
miaka mitano. Unagharimu shilingi bilioni 222. Hiki ni kioja kingine!
Maana,
mpaka mradi huu uje ukamilike, basi, yumkini kuna ambao watakuwa
wameusikia mradi na kufa hata bila kuvikamata vitambulisho vyenyewe. Na
pia tujiulize; katika hali yetu ya sasa, mradi wa vitambulisho vya
kitaifa una maana gani?
Na hivi
hakuna mawaziri wetu wenye uthubutu wa kufungua vinywa vyao kwenye kikao
cha Baraza la Mawaziri na kutamka; ”Mh. Rais, tunashauri Mradi wa
Vitambulisho Vya Taifa usitishwe na kuwekwa kando mara moja. Si
kipaumbele chetu kwa sasa. Ni anasa ya baadae. Tuchote fedha zilizobaki
kwenye mradi huo tuziingize katika dharura ya kupunguza hali mbaya ya
umeme tuliyo nayo nchini kwa sasa.”
Ndio,
Mawaziri wetu ndio wenye kuunda Serikali na wana nafasi ya kuwapa ahueni
Watanzania kwa kuwapunguzia mizigo ya matumizi yasiyo ya lazima kwa
sasa kama haya ya kugharamia mradi wa Vitambulisho vya Taifa." Mwisho wa
kunuu nilichoandika 2011.
Itakapofika
Februari 2 mwaka huu, itakuwa imetimu miaka minane tangu Baraza la
Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Nne libariki mradi huu.
Tumepokea
kwa furaha sana hatua hii ya Rais kutumbua jipu hili la NIDA. Swali
linabaki , je, katika hali halisi ya sasa, tuna haja ya kutumia
mabilioni ya shilingi kugharamia mradi uliokwisha? Kwanini visitumike
vitambulisho vya mpiga kura? Au hati za kusafiria. Mradi wa Vitambulisho
vya kitaifa umegeuzwa ' ng'ombe wa maziwa'. Wanyonge walio wengi ndio
ng'ombe wanaokamuliwa. Mradi huu ni anasa inayopaswa kusubiri.
2. Simbachawene amng'oa Mkurugenzi wa Manispaa...
Ni habari
kutoka Dodoma. Ni hatua sahihi, kama Mkurugenzi ameshindwa kuwasimamia
walio chini yake hapaswi kubaki kwenye nafasi hiyo. Ni habari inayopewa
nafasi ya pili na mtandao wa Mjengwablog.com
3. Serikali ' yajitoa' mgogoro wa Zanzibar
Hii nayo
ni habari kubwa inayopewa nafasi ya tatu na mtandao huu. Waziri wa Fedha
Dr. Mpango kaweka wazi hilo jana Bungeni Dodoma. Kwamba wenye jukumu la
kuitafuta suluhu ya Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe.
No comments:
Post a Comment