Habari ya
mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili,
ambayo imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo.
''Hata
mwendawazimu katika mji mkuu wa Asmara atajua kwamba habari hii sio ya
kweli'',afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea Kenya ameiambia BBC.
Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kitengo cha gazeti la The Standard la Kenya cha Crazy Monday.
Baadhi ya
watu wametoa maoni yao katika mtandao wa Twitter kwamba wako tayari
kusafiri hadi Eritrea ili kutafuta wanawake wa kuoa.
''Jarida
la Crazy Monday ambalo huchapishwa na gazeti la Standard hujulikana sana
kwa stori zake za udaku, likiwa ni mpango wa kutaka kuwavutia vijana,"
anasema Mathias Muindi wa BBC Media Monitoring
Lakini
hilo halijazuia taarifa hiyo kuripotiwa katika mataifa ya Nigeria hadi
Afrika Kusini huku wengine wakisema kuwa ni ukweli.
Habari
hiyo inasema kwamba ili kuhakikisha kuwa kuna wanaume walio wachache
nchini humo wanaokidhi mahitaji ya wanawake walio wengi, kufuatia vita
kati ya taifa hilo na Ethiopia mwaka 1998-2000, kila mwanamume lazima
aowe wake wawili la sivyo afungwe jela.
Lakini afisa wa ubalozi wa Eritrea aliyezungumza na BBC amesema idadi ya wanawake na wanaume inakaribiana.
Waziri wa
habari nchini Eritrea Yemane Gebremeskel alituma ujumbe katika mtandao
wa Twitter akisema kwamba habari hiyo ni ya uvumi, sio ya kweli na
inakera
No comments:
Post a Comment