TIMU ya Maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons ya jijini Mbeya imesema ina imani itaendelea kufanya vizuri katika michezo mwendelezo wa Ligi kuu Soka Tanzani Bara ili kujiweka katika nafasi ya kutokushuka daraja.
Prisons ambaayo msimu huu inanolewa na Kocha Salumu Mayanga , katika msimu uliopita wa Ligi ilikuwa miongoni mwa timu zilizo nusurika kushuka Daraja tofauti na mwaka huu ambapo imebadilika na kuonyesha ushindani.
Na katika mechi zilizopigwa Alhamisi vinara Yanga Africans imerejea kileleni baada ya kuibamiza Maji Maji mabao 5-0 yaliyofungwa na Amis Tambwe matatu na Donald Ngoma na Taban Kamusoko, huku Mwadui FC ikiifunga Kagera Sugar 2-1, Na African Sports na Mtibwa Sugar zikitoka bila kufungana.
Kocha wa Timu hiyo Salum Mayanga amesema kama ilivyo kwa michezo mingine, Soka ni mchezo wa makosa hivyo makosa waliyo yafanya Cost ndiyo yaaliyo wawezesha wao kuibuka na ushindina ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo.
Kwa upande wao mashabiki wa Timu hiyo wamesema , hawakutegemea timu yao kuibuka na ushindi huo kutokana na historia ya Cost union inapocheza Sokoine huku Kocha wa Cost Union kwa upande wake akikataa kuonyesha ushirikiano kwa wanahabari.
Yote kwa yote timu hizo zote haziko katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi.
No comments:
Post a Comment