Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya afya mkoani Mbeya,
mratibu wa uzazi na watoto mkoa wa Mbeya, Prisca Butuyuyu amesema kuwa
utafiti ambao umefanyika unaonyesha kuwa mkoa wa Mbeya unaongoza nchini
kwa kuwa na asilimia 50 ya watoto wenye udumavu wa mwili na akili ukiwa
juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 42.
Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina amesema kuwa tayari
mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali
inayosaidia watu masikini na wenye uhitaji mkubwa, CRS, umeshaandaa
mkakati wa miaka mitano wa kukabiliana na tatizo la udumavu wa mwili na
akili kwa watoto watakaozaliwa, mpango ambao utasaidia kwa kiwango
kikubwa kupunguza tatizo hilo akifungua mkutano huo, katibu tawala mkoa
wa Mbeya, Mariam Mutunguja amesema mkoa wa Mbeya unavyo vyakula vingi
ambavyo vikitumika vizuri hakuna sababu ya kuwepo kwa tatizo la udumavu,
lakini akadai kuwa chanzo cha tatizo ni mila potofu zinazofuatwa na
akinamama wanapopata ujauzito, hivyo akawataka wataalam wa afya
kuwatumia watu maarufu na machifu kufikisha elimu ya kupambana na mila
hizo.
No comments:
Post a Comment