MKAZI
wa kitongoji cha Ilembo katika mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani
Mbeya, Patrick Moses (19) amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka
mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya wizi wa mbuzi mmoja mwenye
thamani ya Sh 85,000.
Hukumu
hiyo imetolewa juzi na Mahakama ya Mwanzo Vwawa mjini, wilayani Mbozi
ambapo Hakimu wa Mahakama hiyo, Lazima Mwaijage alisema ametoa hukumu
hiyo kwa mujibu wa kifungu cha Sheria namba 268.
Awali
imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi
Hamis Mohamed kuwa mnamo Januari 20, mwaka huu saa 11 jioni mshitakiwa
alivamia nyumbani kwa Bahati Mtafya (38) na kuiba mbuzi mmoja mwenye
thamani ya shilingi 85,000 jambo ambalo ni kinyume na Sheria namba 229
sura ya 16 ya kanuni ya adhabu.
Kufuatia
kosa hilo, Mwendesha Mashitaka huyo ameiomba mahakama kutoa adhabu kali
kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wale wenye nia ya kutenda
kosa kama hilo kutokana na wimbi kubwa la vijana kujikita katika wizi na
kuacha kufanya kazi zilizo halali.
Akijitetea
kabla ya kutolewa kwa hukumu, mshitakiwa ambaye tangu awali alikiri
kutenda kosa hilo, aliomba kupunguziwa adhabu akisema anategemewa na
familia yake.
No comments:
Post a Comment