Watu hao wanaripotiwa kufa katika kijiji cha Zashe kata ya Kagunga
katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma huku mva hiyo ikikata mawasiliano
katika vitongoji vya Rusollo, Bukombe na Mlama, ambapo akiongea kwa
njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amekiri
mvua kusababisha vifo na uharibifu huo.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Kigoma ujiji ambako pia mvua
imesababsha madhara makubwa na kuacha familia kadhaa bila ya makazi
pamoja na kuhatarisha majengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jingo la
shirika la nyumba la taifa NHC wamewalalamikia wakandarasi na kuomba
serikali kujenga miundombinu imara ili kuelekeza maji katika ziwa
Tanganyika.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kigoma mjini Hussein Kalyango
amesema ujenzi wa daraja la Stesheni na miradi mingine ya kuwezesha mji
huo kupitisha maji imechelewa na kusababisha adha kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment