Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM Jumatano hii, Mrisho Mpoto alisema hali hiyo iliwafanya watanzania waliohudhuria onesho hilo kumvamia nyuma ya jukwaa na kutaka kujua kwanini alifanya hivyo.
“Mimi nakumbuka niliwahi kuchaguliwa na Kenya ili kujumuika na wasanii wengine wa Uganda na Kenya kufanya onesho la Global Shakespeare,” alisema Mpoto.
“Kuna mwandishi duniani anaitwa William Spears aliteua vitabu vyake 42 vitafsiriwe katika lugha mbalimbali duniani kikiwemo Kiswahili. Vile vitabu baada ya kutafsiriwa akasema vikachezwe kwa lugha zao. Kwahiyo ile kazi walipewa Wakenya, Kenya walivyopata ile tenda wakasema tufanye ‘East African Project’ au mradi wa Afrika Mashariki.
Niliambiwa kwamba tunafanya project ya Afrika Mashariki na nikaoneshwa barua ya kwamba wale ‘Global Shakespeare’ kutoka London wamerecommend kwamba katika kazi hii mtu anayeitwa Mrisho Mpoto asikose. Kwahiyo wale waliniomba mimi nikafanye ile project kama mhusika mkuu ambae ni full staff. Kwahiyo mimi nikaingia mkataba na kampuni ya Kenya theater kama mwakilishi kutoka Tanzania, pia wawakilishi wengine kutoka katika mataifa ya Afrika alisaini mkataba na wote tukafanya mazoezi kwa miezi mitatu nchini Kenya,” alisema.
Aliendelea, “Tulipokuwa London kwenye show yetu ya kwanza ambayo ilihudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali pamoja na watanzania, sisi tukiwa back stage tukiwa tunajiandaa kwa ajili ya kuingia jukwaani kuanza kuigiza kitabu, mimi ni mhusika mkuu ambaye naingia baada ya onesho kuanza. Kwahiyo wale watu waliotangulia kabla ya kuanza mchezo lazima utaimbwa wimbo wa taifa. Kwahiyo katika kuimba wimbo wa taifa, uliimbwa wimbo wa taifa la Kenya na asilimia 90% ya watu walikuwa Wakenya. Kwahiyo baada ya wimbo wa taifa mchezo unatakiwa kuanza, kwahiyo nichague mawili, nisiingie jukwaani au niingie jukwaani kwa sababu ya mkataba halafu nije nihoji kwanini walinifanyia hivyo?@
“Kwahiyo baada ya mchezo watanzania wanaoishi Uingereza wakaja back stage, wakawa wakali wakanikunja na kutaka kunipiga. Lakini bahati nzuri polisi wakaja wakazuia, watu wakawa wamekasirika sana kwanini naimba wimbo wa Kenya wakati mimi ni Mtanzania? Lakini nashukuru Mungu niliongea mpaka kwenye BBC pia tukaenda ukabozi wa Tanzania, nikawaambia hapana mimi nilichezewa faulo, sikuwa na nia hiyo.”
No comments:
Post a Comment