CHAMA
Cha Kijamii (CCK) kimelaani mpango unaofanywa na wabunge wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni, wa kutaka kumng’oa Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia
Ackson na kimewataka kufuata kanuni za uendeshaji wa Bunge.
Hayo
yamo kwenye taarifa ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCK, Constantine Akitanda
aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, iliyotokana na tathmini ya Bunge
tangu kurejeshwa Mfumo wa vyama vingi vya siasa, chanzo na kupevuka kwa
ususaji wa shughuli za Bunge.
Kuhusu mpango wa kutaka kumng’oa Dk Tulia, Mwenyekiti huyo wa CCK alisema; “Hivi
sasa kuna propaganda inayoenezwa ya kutaka kumng’oa Naibu Spika, Dk
Tulia Ackson kwa madai ametumwa na Rais kuminya uhuru na demokrasia
ndani ya Bunge.
“Hii
si mara ya kwanza kwa kambi ya rasmi ya upinzani kulalamikia kiti cha
Spika. Pia si mara ya kwanza kwa kambi hiyo kususa na kutoka nje ya
bunge, pia si mara ya kwanza wabunge wa upinzani kukorofishana na kiti
cha spika na kususa,” alisema.
Akitanda
alisema tatizo la kambi hiyo ni pale spika anaposimamia kanuni huku wao
wakikataa kwa makusudi, kufuata taratibu na kanuni za uendeshaji wa
shughuli za Bunge, jambo alilosema haliwezi kufumbiwa macho.
“Kanuni
zipo wazi kama hujaridhika na maamuzi ya kiti cha Spika unaruhusiwa
kukata rufaa na hoja ikajadiliwa, sasa wabunge wetu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani sijui ni kwa nini hawataki kufuata utaratibu huu, ambao ni wa
kikanuni. Wao wanataka kumng’oa Naibu Spika tu basi, kanuni je?”
Alisema dalili za kukataliwa kwa Naibu Spika na wabunge hao zilionekana tangu mwanzo kwani walimkataa hata kabla ya kuanza kazi kwa madai kuwa ametumwa na Ikulu, na hata siku ya kujieleza akiomba kura alikuwa anazomewa na wabunge wa kambi hiyo.
Alisema dalili za kukataliwa kwa Naibu Spika na wabunge hao zilionekana tangu mwanzo kwani walimkataa hata kabla ya kuanza kazi kwa madai kuwa ametumwa na Ikulu, na hata siku ya kujieleza akiomba kura alikuwa anazomewa na wabunge wa kambi hiyo.
“Kimsingi
tangu mwanzo wabunge wetu wa upinzani hawakumtaka Dk Tulia kutokana na
umahiri wake wa kuzijua na kuzisimamia kanuni kwa ustadi mkubwa.”
Akitanda alisema tangu Bunge la vyama vingi lianze mwaka 1995, wabunge wa upinzani kutokana na uchache wao wamekuwa wanalalamikia kiti cha Spika na kutofautiana na Spika au kudai wanaburuzwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akitanda alisema tangu Bunge la vyama vingi lianze mwaka 1995, wabunge wa upinzani kutokana na uchache wao wamekuwa wanalalamikia kiti cha Spika na kutofautiana na Spika au kudai wanaburuzwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema
katika kipindi cha mwaka 2010 hadi sasa ambapo Chadema kwa mara ya pili
imetoa kiongozi wa upinzani bungeni, nchi imeshuhudia wabunge wa
upinzani wakitumia muda mwingi kulalamikia kiti cha Spika.
“Kwa
kipindi cha 2010 hadi 2015, Spika wa Bunge alikuwa Anne Makinda na
Naibu Spika Job Ndugai. Wapinzani walimlalamikia sana spika wakimtuhumu
kuwa anailinda serikali na kuwa kiti cha Spika kimemshinda."
Alisema
picha ambayo Watanzania wanaipata kutoka kwa Kambi Rasmi ya Upinzani
yenye nia ya kumng’oa Dk Tulia kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani
naye, ni mwendelezo wa wazi wa udhalilishaji wa wanawake kuwa hawana
uwezo wa kuongoza.
No comments:
Post a Comment