Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema vitendo vya unyanyasaji
wapinzani vinavyoendelea nchini ni maradhi yanayokikumba chama tawala.
Maalim
Seif aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano uliondaliwa na Kituo
cha Elimu cha Kimkakati cha Kimataifa cha Marekani (CSIS) juzi,
uliofanyika Washington DC nchini Marekani.
Akizungumzia
kukandamizwa kwa wapinzani nchini, Maalim Seif alitoa mfano wa yeye
kuhojiwa na polisi 11 kwa saa tatu na kijana aliyehukumiwa kifungo cha
miaka mitatu au kulipa faini ya Sh7 milioni kwa kumkosoa Rais John
Magufuli kwenye ukurasa wa facebook.
Kadhalika
alitoa mfano wa viongozi wa Chadema kuhojiwa polisi na baadhi kuwekwa
rumande kwa saa kadhaa huku kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo naye
akihojiwa kwa kufanya mkutano.
“Tunashuhudia mmomonyoko wa hali ya juu wa demokrasia sasa hivi… na hali hii itazidi miezi michache ijayo,” alisema.
Alisema wapinzani wanakandamizwa zaidi upande wa Zanzibar, na kusema kuwa CUF inataka ufafanuzi wa Muungano na wala si kuufuta.
Kiongozi huyo wa CUF alimlaumu Rais John Magufuli na kusema licha ya kuwa nchi za nje zinamuona anafanya vyema katika kupambana na rushwa, lakini Wazanzibari hawana furaha na uongozi wake.
Kiongozi huyo wa CUF alimlaumu Rais John Magufuli na kusema licha ya kuwa nchi za nje zinamuona anafanya vyema katika kupambana na rushwa, lakini Wazanzibari hawana furaha na uongozi wake.
“Kuna
mitazamo tofauti hasa kwa walio nje ya Tanzania kwamba anapambana na
rushwa, lakini kama kiongozi wa nchi, ameshindwa kufanya majukumu yake
kuhusu Zanzibar,” alisema
Alisema mara zote Rais Magufuli anapoulizwa kuhusu suala la Zanzibar, husema hawezi kuchukua hatua.
Alisema mara zote Rais Magufuli anapoulizwa kuhusu suala la Zanzibar, husema hawezi kuchukua hatua.
“Wazanzibari wanachokitaka ni kuona Rais Magufuli anawajibika kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema
Maalim Seif ambaye katika mkutano huo, aliambatana na mkurugenzi wa
Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu na katibu wake, Issa Kheri
Hussein.
Pamoja
na mambo mengine, Maalim Seif alisema chama chake kipo tayari kufanya
uchaguzi mwingine, endapo utasimamiwa na taasisi za kimataifa
zisizofungamana na upande wowote.
Alisema
wakati wakisubiri hilo, wafuasi wa chama hicho wanaendelea kufanya
mgomo baridi usio na nia ya vurugu ili kuonyesha kuwa mambo hayawezi
kwenda kama kawaida.
Akijibu
swali la mmoja wa waliohudhuria mkutano huo kuhusu kutuhumiwa kuuvunja
Muungano endapo atakuwa Rais wa Zanzibar, Maalim alisema chama tawala
kimekuwa kikivibatiza vyama vya upinzani majina ya uongo ili kuvibomoa.
“Kuna
wakati walikiita CUF kuwa ni chama cha Kiislamu, lakini hilo si kweli,
tumenyang’anywa ushindi zaidi ya mara tano na wala hatujaleta fujo,” alisema.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast,
Maalim alielezea jinsi uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ulivyofutwa na
kusema kuwa CUF imekuwa ikinyang’anywa ushindi tangu mfumo wa uchaguzi
wa vyama vingi uanze mwaka 1995.
“Tumefanya
chaguzi tano, 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 katika chaguzi zote hizi,
watu wa Zanzibar waliichagua CUF kuongoza Serikali. Lakini CUF imenyimwa
kushika madaraka,” alisema Maalim na kuongeza:
“Kuna harufu ya hatari, kwa miaka yote hiyo tumejitahidi kuwatuliza wafuasi wetu, tumeangalia namna ya kuzungumza na wenzetu ili waheshimu maamuzi ya watu, lakini hawasikii.”
“Kuna harufu ya hatari, kwa miaka yote hiyo tumejitahidi kuwatuliza wafuasi wetu, tumeangalia namna ya kuzungumza na wenzetu ili waheshimu maamuzi ya watu, lakini hawasikii.”
Alisema
uchaguzi wa mwaka jana ulifanyika kwa uhuru na haki na matokeo
yalionyesha kuwa CUF kimeshinda, lakini polisi waliizingira Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na baadaye Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha
Salim Jecha akayafuta matokeo hayo.
Alisema
hata Umoja wa Ulaya (EU) walitoa ripoti yao wiki mbili zilizopita,
iliyoonyesha kuwa ZEC haikuwa na mamlaka ya kufuta matokeo hayo.
“Nilijaribu
kuwasiliana na Dk Ali Mohamed Shein , lakini hakutaka kupokea simu
yangu, lakini baadaye nilimuandikia barua nikitaka mazungumzo naye,
alikubali kwa masharti kuwa wawepo watu wengine.”alisema na kuongeza: “Tukakubaliana
tufanye mazungumzo, lakini wawepo viongozi wakubwa, wakati tukiendelea
na mazungumzo, Jecha alitangaza kuwa uchaguzi utarudiwa Machi 20.”
Maalim
Seif alitaja athari za kufutwa kwa uchaguzi huo kuwa ni pamoja na
kuvunja maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar na Maamuzi ya Wazanzibari
wengi walioamua nchi yao iongozwe kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa (SUK).
Alitaja
athari nyingine kuwa ni kuwarudisha nyuma watu wa visiwa vya Unguja na
Pemba, kuibuka kwa siasa za chuki, migogoro na kubaguana.
“Hayo
ni pamoja na kudhoofika kwa sekta za uchumi, biashara, ukosefu wa ajira
na maendeleo kwa jumla, na siyo kwa Zanzibar pekee bali kwa Jamhuri
yote ya Muungano wa Tanzania, hasa iwapo Mataifa yataitenga na kulinyima
Taifa misaada, hali ambayo haiwezi kuepukika”. alisema
Akieleza
msimamo wa waandaaji wa mkutano huo, uliojumuisha marais mbalimbali
wastaafu wa Marekani na Ulaya, Mkurugenzi Mkuu wa NDI, Peter Craig
aliwataka viongozi wa kisiasa wa nchi nyingine za Afrika kuiga mwenendo
wa Maalim Seif.
“Tunaomba
watu wengine wenye migogoro ya aina hii waige mfano huu wa Seif Sharif
Hamad na sisi tutakuwa pamoja nao mpaka haki itendeke na ipatikane na
tukianzia na Zanzibar,” alisema
No comments:
Post a Comment