Ofisi ya Rais Ikulu imewanyima vibali vya kusafiri kwenda Marekani wabunge wawili wa Kambi ya Upinzani, bungeni na kumruhusu mbunge wa Geita Mjini (CCM), John Kanyasu.
Wabunge hao wa kambi ya upinzani waliochaguliwa kwenda Marekani ni Savelina Mwijage (CUF) na Mwita Mwaikabwe (Chadema)
Wabunge
hao watatu ni wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi, lakini baada ya
kunyimwa vibali hivyo wamejitoa kwenye kamati hiyo wakipinga kitendo
hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, mbunge wa Ukonga
(Chadema), Mwita Mwikwabe alisema walipata barua ya kuteuliwa kushiriki
safari hiyo kutoka Ofisi ya Bunge Mei 24.
“Tunapenda
kukufahamisha kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amekuteua
kushiriki mkutano wa ngazi ya juu ya maamuzi kuhusu Ukimwi duniani
utakaofanyika 08-10 New York, Marekani,” alinukuu barua hiyo iliyosainiwa na Patson Sobha kwa niaba ya Katibu wa Bunge.
Katika barua hiyo wametajwa wabunge wengine kwenye safari hiyo kuwa ni mbunge wa viti maalum (CUF), Savelina Mwijage.
“Nikiwa
Tarime nilipata simu kutoka kwa Patson kwamba, Naibu Spika alipokea
simu kutoka Ikulu kuwa imezuia vibali vyetu vya kwenda Marekani na
badala yake Kanyasu ameteuliwa,” alisema Mwikabe.
“Tunashangaa, kuteuliwa tuliambiwa kwa barua, lakini kukataliwa tuliambiwa kwa simu,” alisema Mwita.
Alisema kutokana na kutopewa kibali, wajumbe wote wa kambi hiyo wamejitoa kwenye Kamati ya Bunge ya Ukimwi.
“Hayo yote yanafanyika kwa sababu Naibu Spika hatupendi kabisa wabunge wa upinzani ndiyo maana wametufanyia haya,” alisema.
Kwa
upande wake, mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alisema
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaambia katika mkutano wa wabunge wote
kuwa hawahusiki katika uombaji wa vibali kutoka Ikulu.
“Mimi mwenyewe nimeshawahi kusafiri zaidi ya mara tatu mbona sijawahi kuomba kibali kutoka Ikulu?” alihoji Mbatia.
Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alihoji kama wabunge hao ndiyo wenye
haki ya kusafiri. Pia alihoji haraka waliyonayo wabunge hao wakati
walishapeleka malalamiko yao kwa maandishi dhidi ya Naibu Spika, Dk
Tulia Ackson.
“Kwani
wanaharaka gani wao? Si walishapeleka malalamiko hayo na yapo kwenye
kamati. Wasubiri uamuzi ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge),” alisema.
No comments:
Post a Comment